Euro 2024: England Wanaenda Kama 'Kichwa cha Mwendawazimu'

Wakiwa na kikosi kilichosheheni mastaa kama Harry Kane wa Bayern Munich, Jude Belingham wa Real Madrid na Phil Foden wa Machester City, pamoja na kupangwa katika kundi dhaifu za Denmark, Serbia na Slovekia hakuna ambae hakuwatazamia Uingereza kufanya makubwa pengine hata kuwa mabingwa wa Euro 2024, ndoto ambazo zinaenda zikififia kila waingiapo uwanjani.

Jude Belingham

Japo mpaka sasa England wanaongoza kundi lao wakiwa na alama 4, wanakosolewa na mashabiki wao duniani kote kutokana na ukweli kwamba wangeweza kufanya vizuri zaidi na kuwa tayari wamejihakikishia kucheza 16 bora kama wangeshinda mechi yao dhidi ya Denmark.

Kikosi hicho cha Southgate kikilazimishwa sare na Denmark katika mchezo uliochezwa Juni 20 licha ya kutangulia kupata goli la mapema liilofungwa na Harry Kane, goli ambalo badala ya kuwafanya wawe bora liliwadidimiza kwani timu ikaanza kucheza kwa kujilinda zaidi hali iliyopelekea waalike mashambulizi zaidi dhidi yao na hatimaye Denmark kufanikiwa kusawazisha kupitia Morten Hjulmand.

Sio Miongoni mwa Timu Vigogo Tena!

England walicheza mechi yao ya kwanza dhidi ya Serbia na kufanikiwa kupata ushindi mwembamba wa goli 1 bila, asante kwa Jude Belingham.

Licha ya ushindi huo, mbinu za kocha Gareth Southgate zilikosolewa na wadau mbalimbali wa soka wakibainishwa kwamba timu hiyo haichezi soka la kushambulia kwa mipango na kasi ikilinganishwa na majina makubwa ya wachezaji wanaounda kikosi hicho.

Mechi ya jana dhidi ya Denmark imezidisha maswali zaidi juu ya uwezo wa timu hiyo.

England walishindwa kabisa kuwapa ‘presha’ Denmark wakiwa na mpira, na hata walipoupata wao walishindwa kufanya mashambulizi mengi ya kutisha kuwawezesha kupata ushindi licha ya nafasi kadhaa muhimu walizozitengeneza na kushindwa kuzitumia vizuri.

Ukiwatazama England wakicheza huoni muunganiko wowote kati ya safu za ulinzi, kiungo na ushambuliaji na matokeo yake Denmark wakawa na kazi rahisi ya kufikia lango la England mara kwa mara.
Msimamo wa Kundi C

Licha ya kwamba wanaongoza kundi C wakiwa na alama zao 4, licha ya kwamba wanaweza kushinda mechi yao ijayo dhidi ya Slovekia na kufuzu hatua ya 16 bora au hata hatua za mbele zaidi, lakini England sio timu itakayoweza kuzisumbua timu vigogo kwenye mashindano kama Ujerumani, Hispania au Ufaransa.

Engaland ni timu nyingine tu ya daraja la kati kama zilivyo Poland, Croatia na Uturuki.

Na Luck Mwaifuge

Post a Comment

Previous Post Next Post