Timu ya taifa ya Serbia iliyo Kundi C katika mashidano ya Euro 2024 pamoja na timu za England, Denmark na Slovekia imetishia kujiondoa katika mashindano hayo iwapo Shirikisho la Mpira Barani Ulaya halitoziadhibu timu za Croatia na Albania kwa kile ilichokiita ‘ushangiliaji wa kukera’ katika mechi iliyozikutanisha timu hizo mbili Juni 19 mjini Hamburg.
Hayo yamebainisha na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira Serbia, Jovan Surbatovic, aliethibitisha kwamba tayari wamepeleka malalamiko rasmi UEFA wakitaka hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya timu hizo hasa kutokana ushangiliaji wao “ua, ua, ua mserbia” katika mechi yao hiyo iliyotamatika kwa sare ya magoli 2-2.
“Hatujafurahishwa na kilichotokea na tutawaomba UEFA wachukue hatua, hata kama itamaanisha timu hizo zisiendelee tena na mashindano” alisema Surbavotic na kuongeza, “kama UEFA wasipowaadhibu tutafikiria iwapo tutaendelea na mashindano.”
Jovan Surbatovic, katibu mkuu wa FSS |
Ikumbukwe kwamba tayari Serbia wameshakutana na adhabu ya UEFA katika Euro 2024 na wangependa kuona hilo likitokea kwa timu zingine zilizofanya makosa sawa na wao. Baada ya mechi yao ya kwanza dhidi ya England, ambayo ilitamatika kwa Serbia kupokea kichapo cha goli 1 - 0, walilazimika kulipa faini ya dola za kimarekani 16,800 kama adhabu ya mashabiki wao kurusha vitu uwanjani.
Na Luck Mwaifuge
Post a Comment