Fabian Hurzeler amekuwa meneja mdogo zaidi kwa kipindi hiki katika ya Ligi Kuu ya Uingereza baada ya Brighton kutangaza Jumamosi kuwa wamemteua kocha huyo mwenye umri wa miaka 31 kama kocha wao mkuu mpya.
Hurzeler, ambaye aliiongoza St Paul kunyakua taji la ligi ya daraja la pili la Ujerumani Bundesliga msimu uliopita, ametia saini mkataba na klabu hiyo ya pwani ya kusini hadi 2027. Hurzeler mzaliwa wa Texas sasa atakuwa akisimamia kikosi cha Seagulls ambapo wachezaji kadhaa, akiwemo James Milner, 38, Danny Welbeck, 33, na Lewis Dunk, 32 wote wanamzidi umri. Lakini mwenyekiti wa Brighton Tony Bloom alisema kazi ya Hurzeler katika kuipeleka St Paul kwenye ligi kuu ya Ujerumani ilimfanya kuwa "mgombea bora" kuchukua nafasi ya Roberto De Zerbi, ambaye aliondoka kwenye Uwanja wa Amex mwishoni mwa msimu uliopita. Hurzeler ataanza kazi yake mpya atakapopokea kibali cha kufanya kazi kabla ya kikosi cha Brighton kuanza maandalizi ya kabla ya msimu mpya Julai.
Post a Comment