Mkeka wa Leo Tarehe 24 Julai 2024: PAOK Watashinda Dhidi ya Borac Banja Luka


Katika mchezo wa raundi ya pili ya kufuzu Ligi ya Mabingwa, PAOK ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Ugiriki watakuwa wenyeji wa mabingwa wa Ligi Kuu ya Bosnia Herzegovina, Borac Banja Luka kwenye Uwanja wa Stadio Toumbas leo Jumatano. Wenyeji hawashiriki katika raundi ya kwanza ya kufuzu Ligi ya Mabingwa, na hivyo mchezo huu wa leo utakuwa wa kwanza wa kimashindano kwao msimu huu.

Borac wao waliwashinda Egnatia Rrogozhine kwenye hatua ya kwanza ya kufuzu Ligi ya Mabingwa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti baada ya kushinda mchezo wa kwanza 1-0 mnamo Julai 10, kabla ya kupoteza mchezo wa pili 2-1 mnamo Julai 17.

Mechi hii inatazamiwa kuwa ya upande mmoja kwa PAOK kushinda kirahisi dhidi ya timu hii ambayo haijawahi kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa. Kitu kingine kinachowapa wenyeji uwezekani mkubwa wa kushinda mechi hii ni sajili nzuri walizozifanya msimu huu wa joto, akiwemo kipa Antonis Tsiftsis, mabeki wa kati Tomasz Kedziora na Konstantinos Thymianis, beki wa kushoti Filipe Soares na kiungo Mady Camara.

Huu hapa chini ni utabiri wetu katika mechi hiyo na nyingine nyingi:

Soko la 1X2 (Home/Draw/Away)

● PAOK - Borac Banja Luka (1) ✅
● Ludogorets – Din. Minsk (1) ✅
● Dinamo B. – Decic (1) ❌


Soko la Magoli (Juu ya/Pungufu ya)

● PAOK – B.B. Luka (Juu ya 2.5) ✅
● Celje – Slovan B (Juu ya 1.5) ✅
● Struga – Pyunik (Juu ya 1.5) ✅
● Riga FC – Slask (Chini ya 3.5) ✅

Post a Comment

Previous Post Next Post