Ed Sheeran Anunua Hisa Katika Klabu ya Ipswich Town

 

Ipswich Town wamerejea kwenye Ligi ya Kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza tangu 2002 na wataanza mbio zao dhidi ya Liverpool Jumamosi tarehe 17 Agosti, 2024 katika uwanja wa Portman Road

Kabla ya mchezo huo, imetangazwa kuwa Ed Sheeran amenunua hisa ndogo katika klabu hiyo. 

Nyota huyo maarufu wa muziki Ed Sheeran amenunua hisa chache katika klabu ya Ipswich Town inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza. Sheeran, 33, alikulia Suffolk na ni shabiki wa Ipswich maisha yake yote. Amekuwa mfadhili mkuu wa jezi za timu za wanaume na wanawake tangu 2021 na amehudhuria michezo kadhaa wakati huo.

Sasa amenunua hisa 1.4% katika klabu kabla ya mechi yao ya ufunguzi wa msimu wa Ligi Kuu dhidi ya Liverpool Jumamosi, Agosti 17. 

"Ni ndoto ya shabiki yeyote wa soka kuwa mmiliki wa klabu anayoishabikia, na ninajisikia kushukuru sana kwa nafasi hii," alisema Sheeran. 

 

Klabu ya Ipswich imesema atakuwa na nafasi ya kukaa katika sehemu maalum ya watu muhimu (executive box) katika uwanja wa Portman Road, lakini hatajiunga na bodi ya timu hiyo kwa kuwa amefanya uwekezaji mdogo tu wa kupita. 

Sheeran aliongeza: "Nimeishi Suffolk tangu nikiwa na umri wa miaka mitatu na, ninaposafiri ulimwengu na wakati mwingine kujisikia kama mgeni katika miji mikubwa, Suffolk na Ipswich daima wamenifanya nijisikie sehemu ya jamii na salama.

"Ni furaha sana kuwa shabiki wa Ipswich Town. Kuna kupanda na kushuka lakini mpira wa miguu ni kukubaliana na matokeo yote. Mimi sio mwanahisa wa kupiga kura au mjumbe wa bodi, hii ni mimi tu kuweka pesa katika klabu ninayoipenda na wao kurudisha fadhila, kwa hivyo tafadhali usinibane na mapendekezo ya usajili au mbinu za kucheza. 

"Nina furaha kwa Ligi Kuu kuanza wikendi hii. Twende pamoja." alimaliza Sheeran.

Post a Comment

Previous Post Next Post