Virgil van Dijk alisema Liverpool walifurahia kipindi cha "kizuri" chini ya Jurgen Klopp, ambaye aliisaidia klabu hiyo kushinda taji lao la kwanza la Ligi Kuu ya Uingereza baada ya miaka 30 mnamo 2020, lakini akasema timu hiyo inapaswa kuzingatia kutengeneza historia yao wenyewe na Arne Slot.
Nahodha wa Liverpool Virgil van Dijk amesisitiza kuwa klabu hiyo lazima izingatie maisha baada ya Jurgen Klopp baada ya kupata ushindi mfululizo kwenye Ligi ya Kuu chini ya kocha mpya Arne Slot dhidi ya Brentford.
Wekundu hao walionekana kuwa hatari katika mchezo wa kwanza wa Slot kwenye Uwanja wa Anfield huku mabao ya Luis Diaz na Mohamed Salah yakiipa ushindi wa 2-0 na kutoa matumaini kwamba Mholanzi huyo anaweza kuiga mafanikio ya Mjerumani Klopp.
Beki huyo wa kati alisema timu haiwezi "kusahau" kile walichopata chini ya Klopp lakini alidai ni muhimu kuzingatia kufanya kazi kwa bidii na Slot na kutengeneza historia zaidi chini ya uongozi wake.
"Wakati na Jurgen ulikuwa mzuri na wakati na bosi mpya ni furaha na ana njia fulani ya kucheza," aliiambia Sky Sports. "Tunafanyia kazi mambo mengi mazuri na unaona mengi ukiwa na mpira au bila mpira ambayo yanaipa timu imani.
"Inatubidi, sitasema kusahau kipindi cha Jurgen, lakini hayo ni mambo ya nyuma na tulikuwa na wakati mzuri na sasa ni wakati wa bosi mpya kufanikiwa. Ndio maana tunapaswa kuzingatia. kwamba, kusiwe na ulinganisho na mambo haya yote kwa maoni yangu.
"Hatuna wachezaji wapya hadi sasa lakini ni wazi nina jukumu la ziada kwa sababu najua wachezaji ndani na nje. Lakini niko hapa kwa ajili yake [Slot]. Nilimwambia kwamba kuanzia siku ya kwanza nitawasaidia na benchi la ufundi, nataka kufanikiwa na tuko kwenye mashua moja.
Timu hiyo itakabiliwa na mtihani mzito wa kujipima kuona wamefikia kiwango gani chini ya Slot, Wekundu hao wanatarajiwa kusafiri hadi Old Trafford kumenyana na wapinzani Man United wiki ijayo.
Post a Comment