Leo Jumatano, Septemba 18 2024, ni siku ambayo wanafainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uiopita Borussia Dortmund watakabiliana na mabingwa wa Ubelgiji, Club Brugge. Wakiwa walikaribia kuchukua taji hilo la UEFA na kuishia fainali msimu uliopita, Dortmund wanatamani kuendeleza walipoishia , wakati Brugge wao wakitaka kujijenga katika taswira ya soka la Ulaya.
Safari ya Dortmund hadi fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu uliopita haikuwa ya kawaida. Licha ya kukabiliwa na kundi gumu hatua ya makundi, ikipangwa na timu kama PSG, AC Milan na Newcastle, ilifanikiwa kuongoza kundi hilo kwa kukusanya pointi 11!
Hata hivyo, fomu yao katika ligi ya ndani ilikuwa tofauti kabisa na mafanikio yao ya Ulaya. Dortmund walimaliza nafasi ya tano katika Bundesliga! Hata hivyo, ushiriki wa mafaikio wa Dortmund katika UEFA uliipatia Ujerumani nafasi ya ziada katika Ligi ya Mabingwa.
Chini ya uongozi wa kocha mpya Nuri Sahin, Dortmund imedhamiria kurekebisha mapungufu yao katika Bundesliga huku wakitaka kudumisha ushindani wao katika UEFA. Sahin, ambaye ni mchezaji wa zamani wa Dortmund, anatarajiwa kuleta utajiri wa mbinu na maarifa katika kikosi cha Dortmund na mwanzo wake umekuwa na matokeo chanya.
Club Brugge, kwa upande mwingine, wanatamani kufanya makubwa katika Ligi ya Mabingwa. Mabingwa hao wa Ubelgiji tayari wamejijengea utawala katika ligi ya ndani, lakini utendaji wao kimataifa umekuwa wa kawaida sana. Msimu uliopita walishindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa lakini angalau walikua na muendelezo mzuri katika Europe Conference League ambapo walifanikiwa kufika hatua ya nusu fainali na kutolewa na Fiorentina.
Mchezo kati ya Dortmund na Brugge unatarajiwa kuwa wa kusisimua. Timu zote mbili zina vikosi vyenye vipaji na zina uwezo wa kutafuta matokeo. Uwezo wa kushambulia wa Dortmund utakuwa kwenye mtihani dhidi ya ulinzi wenye nguvu wa Brugge, wakati uwezo wa kushambulia wa Brugge utakuwa tishio kwa lango la Dortmund.
Takwimu Muhimu:
*Msimu uliopita katika UEFA Dortmund walicheza mechi 6 za ugenini wakishinda 3, sare 1 na kupoteza mara 2 (dhidi ya PSG na Atletico Madrid)
*Dortmund wamefanikiwa kufunga magoli mawili au zaidi kaika mechi 3 kati ya 4 msimu huu
Ubashiri wetu leo katika mechi hii Borussia Dortmund kushinda
Angalia mkeka zaidi hapa chini
MATOKEO NDANI YA DAKIKA 90
⚽PSG – Girona: 1 ✅
⚽Club Brugge - Borussia Dortmund: 2 ✅
⚽Celtic - Slovan Bratislava: 1 ✅
⚽Coventry City - Tottenham: 2 ✅
⚽Ajax - Fortuna: 1 ✅
⚽Oster - Trelleborg: 1 ✅
JUU/CHINI [OVER/UNDER]
⚽Sparta Praha - Salzburg: Over 1.5 ✅
⚽Manchester City - Inter: Over 1.5 ❌
⚽PSG – Girona: Over 1.5 ✅
⚽Celtic - Slovan Bratislava: Over 1.5 ✅
⚽Real Betis - Getafe: Under 3.5 ✅
⚽Nomme Kalju - Nomme United: Over 2.5 ✅
Post a Comment