Rebecca Cheptegei enzi za uhai wake |
Mkimbiaji wa marathon wa Olimpiki Rebecca Cheptegei, aliyeuwawa na mpenzi wake wa zamani, amezikwa katika shamba la baba yake mashariki mwa Uganda.
Akiwa kama mwanachama wa vikosi vya ulinzi vya Uganda, Rebecca alipewa heshima ya kuzikwa kijeshi.
Dickson Ndiema, mpenzi wa zamani wa Cheptegei, ndiye aliemuua Rebecca kwa kumshambulia kwa petroli karibu na nyumba yake akimwacha na majeraha makubwa ya moto ambayo hatimaye yalimfanya afariki. Mauaji ya kikatili ya mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 33 yalishtua ulimwengu wa michezo.
Katika mazishi ya Cheptegei huko Bukwo, wanariadha wenzake walivaa T-shirt nyeusi zenye kauli mbiu “sema hapana kwa vurugu za kijinsia” huku waziri wa Michezo na Vijana wa Kenya, Kipchumba Murkomen, akikubali alisisitiza umuhimu wa kushughulikia masuala ya msingi.
Wakati wa mazishi, viongozi wa eneo hilo walifanya ibada ya mazishi, wakipendekeza barabara na eneo la michezo kupewa jina la mwanariadha huyo kwa heshima ya mchango wake katika michezo.
Cheptegei alifariki dunia hospitalini siku nne baada ya shambulio hilo kutokana na majeraha makubwa ya moto. Huku Ndiema, ambaye pia alijeruhiwa katika tukio hilo akifariki dunia baadaye.
Mchungaji wa kanisa ambalo Cheptegei alikua akisali, Caroline Atieno, alimtaja kama mtu mzuri na mchaji Mungu. Alifanya mazungumzo na Cheptegei wakati akiwa hospitalini, ambapo mwanariadha huyo alionyesha kutoamini kwake tukio hilo na hasira kwa mshambuliaji wake.
Ibada ya mazishi ilifanyika huko Eldoret, Kenya, kabla ya mwili wa Cheptegei kusafirishwa kwenda Uganda. Mama yake, Agnes Cheptegei, alivaa T-shirt iliyo na kauli mbiu “kuwa mwanamke haipaswi kuwa hukumu ya kifo.”
Kifo cha kikatili cha Cheptegei kiliashiria mauaji ya tatu ya mwanariadha wa kike nchini Kenya katika kipindi cha miaka mitatu. Katika kila kesi, wapenzi wa sasa au wa zamani walihusishwa kama washukiwa.
Vurugu dhidi ya wanawake imekuwa tatizo kubwa nchini Kenya. Uchunguzi mwaka 2022 ulibaini kuwa angalau asilimia 34 ya wanawake waliathirika na vurugu za kimwili.
Post a Comment