Adhabu ya Paul Pogba Kupunguzwa hadi Miezi 18, Kurudi 2025

Kiungo wa Juventus, Paul Pogba, ameripotiwa kuwa adhabu yake ya kutumia dawa za kuongeza nguvu imepunguzwa kutoka kufungiwa miaka minne hadi miezi 18, ikimaanisha kwamba kurejea kwake uwanjani sasa kunakaribia zaidi kuliko ilivyotarajiwa.


Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 31 hajasakata kabumbu tangu mwanzoni mwa msimu wa 2023-24. Alicheza mechi mbili kati ya mechi tatu za kwanza za Juventus za Serie A, na mechi yake ya mwisho ilikuwa tarehe 3 Septemba 2023 dhidi ya Empoli. Kabla ya mechi hiyo.

Pogba alikuwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumika kwenye mechi ya ufunguzi ya Juventus dhidi ya Udinese, ambapo alifanyiwa vipimo vya dawa za kusisimua mwili vilivyoonesha viwango vya juu vya homoni ya testosterone. Kipimo cha pili kilithibitisha viwango vya juu vya homoni hiyo, jambo lililomfanya apate adhabu ya kufungiwa kwa miaka minne na Mahakama ya Taifa ya Dawa za Kusisimua ya Italia mwezi Februari 2024.

Pogba alikata rufaa dhidi ya uamuzi huo katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), ambayo sasa imepunguza adhabu hiyo hadi miezi 18. Kwa kuwa alifungiwa kuanzia Septemba 2023, mshindi huyo wa Kombe la Dunia ataweza kurejea kwenye mechi za ushindani kufikia Machi 2025. Pogba pia ataweza kuanza mazoezi na Juventus mapema Januari 2024.

Mahakama ya CAS imeripotiwa kugundua kuwa Pogba alitumia kwa bahati mbaya dawa ya Dehydroepiandrosterone (DHEA), ambayo husaidia kuongeza testosterone, ingawa ina athari kubwa kwa wanawake na haikumsaidia kupata faida isiyoruhusiwa.

Kama adhabu ya awali ingesimama, Juventus walitarajiwa kuvunja mkataba wake, hali ambayo ingeweza kumlazimisha kiungo huyo kustaafu mapema. Hata hivyo, kwa adhabu yake kupunguzwa, Pogba atasalia kuwa na mkataba na klabu hiyo hadi majira ya joto ya 2026.

Kabla ya kufungiwa, Pogba alikuwa amecheza mechi 11 tu kwa Juventus tangu kurejea kwake kutoka Manchester United mwaka 2022, akipitia changamoto za majeraha. Kurejea kwake kunaweza kutokea kwenye mechi ya Serie A dhidi ya Fiorentina mnamo Machi 16, 2025.

Post a Comment

Previous Post Next Post