Matumaini ya Ubingwa kwa Arsenal: Saka Anaamini “Huu Ndio Mwaka wa Kufosi”

 
Mshambuliaji wa Arsenal, Bukayo Saka, ana imani kuwa msimu huu The Gunners watavunja ukame wa miaka 21 wa kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza. Baada ya kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Manchester City kwa misimu miwili iliyopita, Saka ana hisia kwamba kampeni hii msimu huu utakuwa tofauti.

Mara ya mwisho Arsenal walitwaa taji la Ligi Kuu ilikuwa mwaka 2003-04 chini ya kikosi cha kihistoria cha Arsene Wenger. Kwa sasa, wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, wakiwa na pointi sawa na Manchester City huku wakizidiwa pointi moja tu na viongozi wa ligi, Liverpool, baada ya mechi sita.

Akizungumza na CBS Sports, Saka alionyesha matumaini yake: 
“Sitaki kuweka shinikizo kubwa kwetu, lakini nadhani huu ndio mwaka [tutashinda taji]. Tumekuwa karibu kwa misimu miwili iliyopita, na tunazidi kusogea karibu. Tunatumaini huu ndio mwaka wetu.”
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anasema uzoefu alioupata kwa kucheza fainali ya Ligi ya Mataifa Ulaya akiwa na England umemchochea kuleta mafanikio Emirates. Ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Paris Saint-Germain katika Ligi ya Mabingwa siku ya Jumanne uliongeza imani yake kwamba Arsenal inaweza kushindana na timu bora za Ulaya.

“Kwa miaka ya nyuma, nimekuwa nikimaliza katika nafasi ya pili mara nyingi. Nina roho ya ushindani inayosukuma kutaka kushinda msimu huu, na naamini katika uwezo wangu,” Saka aliiambia Amazon Prime. “Tunajiamini sisi kama timu, na tulionyesha hilo usiku wa leo dhidi ya PSG. Niliwaambia wachezaji wenzangu kuwa tunahitaji kutoa kauli kubwa timu kubwa zinapokuja Emirates.”

Kwa ari hiyo na imani, Saka na Arsenal wanakusudia kutoa changamoto kubwa katika mashindano ya ndani na Ulaya msimu huu.

Post a Comment

Previous Post Next Post