Samatta Arejeshwa Katika Kikosi cha Taifa Stars Kitakachocheza Mechi ya Kufuzu AFCON 2025 vs DR Congo

 
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Hemed Suleiman, ametangaza kikosi rasmi kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo miwili ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025. Timu ya Taifa Stars itakutana na DR Congo tarehe 10 Oktoba 2024 na 15 Oktoba 2024 katika mechi muhimu za hatua ya kufuzu.

Katika kikosi hiki, nahodha na mshambuliaji nyota Mbwana Samatta amerejeshwa tena baada ya kuwa nje kwa muda. Samatta anayekipiga katika klabu ya PAOK ya Ugiriki, ni mchezaji ambaye ameendelea kuwa tegemeo kwa Taifa Stars kwa miaka mingi, na kurejea kwake kunaleta matumaini makubwa kwa mashabiki wa soka nchini.

Kikosi Kamili cha Taifa Stars

Hawa ni wachezaji walioitwa kwa ajili ya michezo miwili ya kufuzu AFCON 2025 dhidi ya DR Congo:

· Ally Salim (Simba SC)

· Zuberi Foba (Azam FC)

· Yona Amos (Pamba SC)

· Mohamed Hussein (Simba SC)

· Lusajo Mwaikenda (Azam FC)

· Pascal Msindo (Azam FC)

· Ibrahim Hamad (Young Africans)

· Bakari Nondo (Young Africans)

· Dickson Job (Young Africans)

· Abdulrazak Hamza (Simba SC)

· Haji Mnoga (Salford City, Uingereza)

· Adolf Mtasigwa (Azam FC)

· Habib Khalid (Singida Black Stars)

· Himid Mao (Talaal El Geish, Misri)

· Mudathir Yahya (Young Africans)

· Feisal Salim (Azam FC)

· Suleiman Mwalim (Fountain Gate FC)

· Cyprian Kachwele (Vancouver Whitecaps, Canada)

· Clement Mzize (Young Africans)

· Mbwana Samatta (PAOK FC, Ugiriki)

· Kibu Dennis (Simba SC)

· Nasoro Saadun (Azam FC)

· Abdullah Said (KMC FC)

Kocha Hemed Suleiman anaongoza kikosi hiki kilichojumuisha wachezaji wenye uzoefu wa michuano ya kimataifa pamoja na vipaji vya ndani.

Stars itahitaji matokeo mazuri katika michezo hii miwili ili kuweka hai matumaini ya kufuzu kwa AFCON 2025. Mechi ya kwanza itachezwa tarehe 10 Oktoba 2024, na mechi ya marudiano itapigwa tarehe 15 Oktoba 2024.

Kongo na Stars zipo kundi H pamoja na timu za Ethiopia na Guinea, Kongo wakiwa vinara wa kundi hilo na alama zao 6 huku Stars wakishika nafasi ya pili na alama zao 4 katika michezo miwili iliyochezwa mpaka sasa.

Kikosi cha Taifa Stars, kikiwa na mchanganyiko wa wachezaji kutoka klabu za ndani na nje ya nchi, kimejiandaa vilivyo kwa mechi hizi muhimu. Kurejea kwa Samatta kunaleta matumaini ya kufanya vizuri katika michezo ya kufuzu na kuwakilisha vyema nchi kwenye AFCON 2025.

Na Luck Mwaifuge

Post a Comment

Previous Post Next Post