Golikipa huyo mwenye umri wa miaka 22 kutoka Denmark alikuwa kipa chaguo la kwanza wa Villarreal kwa msimu uliopita, akifanikiwa kucheza mechi 37. Jorgensen alionyesha kufurahishwa na dili la kujiunga na The Blues, akisema,
"Kujiunga na Chelsea ni ndoto iliyokuwa kweli. Ninafurahi sana kusaini mkataba na Chelsea, moja ya klabu kubwa duniani. Ninatarajia kukutana na wachezaji wenzangu katika klabu hii na kuanza kucheza pamoja nao.”
Jorgensen anatarajiwa kushindana na Robert Sanchez katika nafasi ya kipa wa kwanza wa Chelsea. Kipa huyo alizaliwa nchini Sweden, na alifanikiwa kuiwakilisha nchi hiyo katika ngazi ya vijana kabla ya kubadilisha uraia wake kuwa wa Denmark akifuata uraia wa baba yake.
Kipa huyo kinda alijiunga na Villarreal akiwa na umri wa miaka 15, akapanda ngazi za vijana hadi kufanikiwa kucheza mechi yake ya kwanza ya wakubwa mwaka 2020 katika kikosi B huku akicheza mechi yake ya kwanza ya La Liga mwezi Januari 2023.
Jorgensen amejiunga na kikosi cha Chelsea
kwenye maandalizi ya msimu mpya nchini Marekani na anaweza kucheza mechi dhidi
ya Club America, Manchester City au Real Madrid kabla ya Chelsea kurudi
Uingereza wiki ijayo. The Blues wanatarajia kuanza kampeni yao ya Ligi Kuu
uwanja wa nyumbani dhidi ya mabingwa Manchester City Jumapili, Agosti 18.
Post a Comment