Simba SC Yawafunga El-Qanah Katika Mechi ya Kirafiki

Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Tanzania,  imeanza kampeni zao za maandalizi ya msimu mpya kwa kishindo baada ya kuichapa El-Qanah SC ya Misri kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Julai 22, 2024 katika uwanja wa Old Suez Canal Stadium. Ushindi huu unawapa Wekundu wa Msimbazi matumaini mazuri kuelekea msimu ujao wa 2024/2025.

Mchezo huu ulikuwa ni sehemu muhimu kwa wachezaji wapya wa Simba kuonesha uwezo wao na kuzoea kucheza pamoja na wachezaji wa zamani katika kikosi hicho. Mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Jean Charles Ahoua, aliibuka kuwa mchezaji bora wa mchezo baada ya kufunga mabao mawili ya haraka katika dakika ya 14 na 16. Mabao ya Ahoua yalionyesha uwezo mkubwa wa kushambulia ambao mshambuliaji huyo anao, na mashabiki watasubiri kwa hamu kuona zaidi kutoka kwa mchezaji huyu mpya msimu mzima ujao.

Mshambuliaji kutoka Nigeria, Augustine Okejepha, alifunga bao la tatu muhimu kwa Simba katika dakika ya 120. Bao la Okejepha lilionesha uwezo wake wa kushambulia  yeye binafsi, lakini pia na timu nzima ya Simba SC.  Kwa kuwa na wachezaji mbalimbali wenye uwezo wa kufunga mabao, Simba inaonekana kuwa tayari kushindana katika michuano mbalimbali msimu ujao.

Kocha mkuu mpya, Fadlu Davids, alitumia mchezo dhidi ya El-Qanah kujaribu mbinu zake za uchezaji na katika hilo timu ilionesha ishara nzuri kwa kufanikiwa kutumia mbinu za Davids kwa ufanisi. Ingawa bado wanaweza kufanya maboresho kadhaa katika kikosi, ushindi huu wa  unaonesha kuwa Simba iko kwenye njia sahihi chini ya kocha wao mpya.

Ushindi huu wa Simba dhidi ya El-Qanah ni kichocheo kikubwa katika kurudisha hali ya kujiamini kwa Simba SC hasa ikizingatiwa kutokana na kuwa na msimu mbaya wa 2023/2024 ambapo walimaliza Ligi Kuu ya Tanzania Bara wakiwa nafasi ya 3 nyuma ya Yanga na Azam.

Post a Comment

Previous Post Next Post