Manchester City imefikia makubaliano ya dau la Pauni milioni 21.2 kumuuza mlinzi wao Joao Cancelo kwenda klabu ya Al-Hilal ya Ligi ya Saudia. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 30 amewatumikia City kwa miaka mitano na sasa anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu na Al Hilal.
Ingawa makubaliano binafsi kati ya mchezaji huyo na Al Hilal bado hayajafikiwa lakini hayatazamiwi kuwa kikwazo katika dili hilo.
Meneja wa City, Pep Guardiola alielezea matumaini kuhusu uwezekano wa Cancelo kurejea katika kikosi cha kwanza cha Manchester City mapema mwezi huu, lakini hata hivyo kutoelewana ambako kulisababisha atolewe kwa mkopo katika timu za Bayern Munich na Barcelona kwa mwaka na nusu uliopita kumekuwa kikwazo kikubwa kwake.
Cancelo amekuwa nje ya mechi mbili za kwanza za City za Ligi Kuu msimu huu na pia alikosa ushindi wa Ngao ya Hisani dhidi ya Manchester United.
Hapo awali, Cancelo alikuwa mchezaji muhimu katika mfumo wa Guardiola. Hata hivyo, muda wake wa kucheza ulipungua katika misimu ya hivi karibuni, na mwishowe kuishia kutolewa kwa mikopo katika timu mbalimbali.
Uhamisho huu kuelekea Saudi Arabia unakuwa muendelezo wa muelekeo wa hivi karibuni wa wachezaji mashuhuri kujiunga na Ligi ya Saudia ikiwa ni pamoja na Cristiano Ronaldo, Karim Benzema, Neymar na Sadio Mane ambao sasa wanakipiga huko Mashariki ya Kati.
Post a Comment