Cristiano Ronaldo alitoka nje ya Uwanja wa Prince Sultan bin Abdul Aziz bila kuchukua medali yake ya fedha baada ya timu yake ya Al-Nassr kuchapwa mabao 4-1 katika fainali ya Saudi Super Cup Jumamosi.
Cristiano Ronaldo (katikati) alikuwa nahodha wa Al-Nassr katika mchezo wa Jumamosi wa Saudi Super Cup dhidi ya Al-Hilal. |
Katika utetezi wake Ronaldo, ni kwamba bao la nne la Al-Hilal lilikuwa ni matokeo ya uzembe wa wachezaji wenzake.
Baada ya majaribio mabaya ya kucheza kutoka nyuma na kusababisha kipa Bento kupoteza mpira kwa Malcom pembeni ya eneo la sita, Ronaldo alisimama katikati ya duara, akaweka mikono yake pamoja na kuwaonyesha wachezaji wenzake kwamba walikuwa 'wamelala'.
Baada ya mchezo huo, wachezaji wa Al-Nassr walikabidhiwa medali kwa kushika nafasi ya pili katika mchuano huo wa timu nne. Lakini nyota wa zamani wa Real Madrid na Man United, Ronaldo hakuwa na nia ya kuchukua yake, hivyo alitoka nje ya uwanja mikono mitupu.
Muda wa Ronaldo pale Al-Nassr umekuwa usiokuwa na utulivu hadi leo.
Rekodi yake ya mabao ni ya kuvutia sana. Sasa amefunga mabao 66 katika mechi 72 akiwa na Riyadh na ameshinda Kiatu cha Dhahabu cha Saudi Pro League msimu uliopita.
Hata hivyo, Al-Nassr walimaliza pointi tano nyuma ya mabingwa Al-Ittihad katika msimu wa kwanza wa Ronaldo - wakiwa kileleni mwa jedwali kabla ya kuwasili kwake - na kisha wakamaliza kwa pointi 14 chini ya Al-Hilal katika kampeni za 2023-24.
Post a Comment