Droo za Ligi za Europa na Conference League zimechezeshwa na sasa kila timu shiriki inajua imepangwa katika kundi gani na wapinzani wake ni nani na nani.
Rangers na Tottenham zimewekwa katika kundi lenye changamoto kwenye Ligi ya Europa ambayo imewekwa katika mfumo mpya. Timu hizi zote mbili zitakabiliana na Manchester United na kisha kukutana zenyewe katika hatua ya makundi.
Ligi ya Europa imepanuliwa ili kujumuisha vilabu 36, vilivyogawanywa katika pots nne za timu tisa tisa. Kila timu itacheza mechi nane dhidi ya wapinzani wanane tofauti.
Manchester United pia itakabiliana na Fenerbahce, Porto, PAOK, Bodo/Glimt, Viktoria Plzen, FC Twente, na FCSB.
Rangers itakabiliana na Lyon, Olympiakos, Union SG, Malmo, FCSB, na Nice.
Tottenham itakabiliana na Roma, AZ Alkmaar, Ferencvaros, Qarabag, Galatasaray, Elfsborg, na Hoffenheim.
Hawa Hapa Wapinzani wa Timu za Uingereza Katika Conference League
Chelsea itakabiliana na Gent, Heidenheim, Astana, Shamrock Rovers, Panathinaikos, Noah, Hearts, na Copenhagen.
The New Saints itakabiliana na Fiorentina, Djurgarden, Astana, Shamrock Rovers, Panathinaikos, Celje, na Dinamo-Minsk.
Larne itakabiliana na Gent, Molde, Olimpija, Shamrock Rovers, St Gallen, na Dinamo-Minsk.
Hatua ya makundi ya Ligi ya Europa itaanza Septemba 25-26 na kuendelea hadi Januari 30. Timu nane bora katika hatua ya ligi zitakwenda moja kwa moja hadi raundi ya 16 bora, wakati timu zilizo nafasi ya tisa hadi ya 24 zitashindana katika raundi ya playoff ili kupata nane zitakazosonga mbele hadi raundi ya 16 bora. Timu 12 za chini katika hatua ya ligi zitatolewa mashindanoni.
Post a Comment