Magoli Mengi Yaliyofungwa kwa Mipira ya Adhabu (Free Kicks) Katika Historia ya Soka


Cristiano Ronaldo amefunga goli lake la 899 kupitia mpira wa adhabu (free kick) katika mechi ya timu yake ya Al Nassr dhidi ya Al Feiha iliyochezwa mnamo tarehe 27 Agosti 2024. Goli hilo lilikuwa miongoni mwa magoli mawili aliyofunga Ronaldo ambayo yalichangia kuiwezesha timu hiyo kuibuka na ushindi wa goli 4 - 1 dhidi ya Al Feiha.

Goli hilo la mpira wa adhabu linamfanya Cristiano Ronaldo kuwa nyuma kwa goli moja kufikia idadi ya magoli yatokanayo na mipira ya adhabu yaliyofungwa na mtabe mwenzake katika soka Lionel Messi. 

Cristiano Ronaldo sasa amefikisha magoli ya free kick 64 wakati Lionel Messi akiwa na 65. Je! Ronaldo atamfikia Messi na pengine hata kumzidi? Au pengine Messi pia atazidi kusogea mbali zaidi kwa kuongeza idadi ya magoli ya free kick? Sisi sote hatujui, muda ndio utakuwa mwamuzi mzuri wa mtanange huo kwani hawa miamba wote bado wanaendelea kulisakata kabumbu katika hatua zao za lala salama.

Ebu tuangalie wachezaji mbalimbali wanaoongoza kufunga  magoli yatokanayo na mipira ya adhabu (free kick)  katika historia ya soka.

7. Cristiano Ronaldo (Portugal)
64 Free Kicks


6. Lionel Messi (Argentina)
65 Free Kicks


5. David Beckham (England)
65 Free Kicks


4. Ronaldinho (Brazil)
66 Free Kicks


3. Victor Legrotaglie (Argentina)
66 Free Kicks


2. Edson Arantes do Nascimento, [Pele] (Brazil)
70 Free Kicks


1. Juninho Pernambucano (Brazil)
77 Free Kicks

Post a Comment

Previous Post Next Post