Juan Izquierdo |
Beki wa Uruguay Juan Izquierdo amefariki dunia baada ya kupata mshtuko wa moyo wakati wa mchezo wa Copa Libertadores mapema mwezi huu.
Izquierdo, mwenye umri wa miaka 27, alianguka uwanjani wakati wa mchezo wa Nacional dhidi ya Sao Paulo mnamo Agosti 22. Licha ya kupata huduma ya kwanza ya matibabu na kulazwa hospitalini, hali yake ilidorora siku za hivi karibuni.
“Ni kwa huzuni kubwa na mshtuko katika mioyo yetu kwamba Klabu ya Nacional inatangaza kifo cha mchezaji wetu mpendwa Juan Izquierdo,” klabu hiyo ilichapisha kwenye mitandao ya kijamii. “Tunatoa pole zetu za dhati kwa familia yake, marafiki, wenzake, na wapendwa Wote. Klabu yote ya Nacional iko katika maombolezo kufuatia tukio hili la kuhuzunisha lililotukuta.”
Habari za kifo cha Izquierdo zimesababisha mshtuko mkubwa katika ulimwengu wa soka. Mshambuliaji wa Inter Miami Luis Suarez alitoa salamu zake za pole akisema, “Maumivu, huzuni, ni vigumu kuelezea. Awe na amani ya milele. Ninawaombea ujasiri kwa familia na marafiki zake katika kipindi hiki kigumu.”
Izquierdo alikuwa mtu maarufu katika klabu ya Nacional na hivi karibuni alikuwa baba kwa mara ya pili kwani mke wake amejifungua siku 10 tu zilizopita. Ligi za Uruguay zimeahirishwa kufuatia tukio hili la kusikitisha.
Post a Comment