Real Madrid Kukabiliana na Liverpool na Dortmund kwenye Ligi ya Mabingwa


Real Madrid, mabingwa watetezi wa Ulaya, wamepangwa katika kundi gumu katika Ligi ya Mabingwa Ulaya liyoandaliwa upya. Wanatarajiwa kukabiliana na Liverpool ugenini na kuwa mwenyeji wa Borussia Dortmund ambao walikutana nao katika hatua ya fainali msimu uliopita.

Ligi ya Mabingwa imetengenezwa upya ili kujumuisha vilabu 36, vilivyogawanywa katika pots nne. Kila timu itacheza mechi nane dhidi ya wapinzani wanane tofauti katika hatua ya makundi.

Real Madrid pia itakabiliana na AC Milan nyumbani na Atalanta ugenini. Liverpool wao watakabiliana na Milan na Girona, na pia watakuwa wenyeji wa Bayer Leverkusen, ambao kocha wake ni Xabi Alonso, mchezaji wa zamani wa Liverpool.

Manchester City, washindi wa Ligi ya Mabingwa mwaka 2023, watacheza na Inter Milan nyumbani na watasafiri kwenda Paris Saint-Germain na Juventus. Pia watakabiliana na Club Brugge, Sparta Prague, na Slovan Bratislava.

Mchezo mwingine muhimu utajumuisha Bayern Munich dhidi ya PSG na dhidi ya Barcelona, na Arsenal dhidi ya Inter Milan na Paris Saint Germain.

Hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa itaanza Septemba 17, 18, na 19. Timu nane bora katika hatua ya ligi zitakwenda moja kwa moja hadi raundi ya 16 bora. Timu zilizo nafasi ya tisa hadi ya 24 zitapitia raundi ya playoff ambayo itaibuka nane zilizobaki zinazosonga mbele hadi raundi ya 16 bora. Timu 12 za chini katika hatua ya ligi zitaondoshwa mashindanoni, na hakutokua na utaratibu wa timu kushuka hadi Europa League kama zamani.

Europa League na Conference League, ambazo droo zake zitafanyika Ijumaa, pia zitajumuisha vilabu 36.

Post a Comment

Previous Post Next Post