David Raya Awabeba Arsenal, Aokoa Penati

Kipa wa Arsenal David Raya ameisaidia timu yake kupata alama moja wakati wakichuana na Atalanta katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kudaka mkwaju wa penalti na kisha rebound ya kichwa , hivyo kuwahakikishia Arsenal sare katika mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa.

David Raya akiokoa Mkwaju wa Penati dhidi ya Atalanta

Mchezo huo, uliopigwa katika Uwanja wa Gewiss Stadium huko Bergamo, Italia, ulishuhudia nafasi chache sana za wazi na ilikua chupuchupu Atalanta wapate goli katika dakika ya 67 kwani walipewa mkwaju wa penati wakati Thomas Partey wa Arsenal akilimwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya Ederson.

Mateo Retegui ndiye aliepewa jukumu la kupiga penati hiyo lakini bahati mbaya kwake pigo lake hilo la upande wa kulia wa Raya lilionekana na golikipa huyo akaufuata mpira kuuzuia usiingie langoni. Retegui alikutana na mpira uliopanguliwa na Raya na akapiga kichwa kizuri sana kuuelekeza langoni, lakini isivyo bahati kwake pigo hilo pia likazuiliwa!

Sare hiyo inawaacha Arsenal na pointi moja katika Kundi A, huku Atalanta pia wakiwa na pointi moja baada ya mchezo wao wa ufunguzi. Timu zote mbili zitakuwa zikitafuta kuboresha nafasi zao katika kundi hilo katika mechi zao zijazo za Ligi ya Mabingwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post