AZ Alkmaar wa moto! Wana hali nzuri hali nzuri wametoka kuwakanda Heerenveen magoli 9-1, wanatarajia kuendelea na mfululizo wao wa kutopoteza mechi katika Eredivisie wakati watakapokutana na PEC Zwolle leo Ijumaa usiku.
PEC Zwolle wao kwa upande mwingine wamekuwa wakipambana kujiweka sawa katika ligi msimu huu, wakiwa na pointi nne tu katika mechi tano za kwanza. Licha ya kuonesha matumaini kiasi waliyoonesha baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Twente hivi karibuni, lakini mpinzani wanaekabiliana nae hivi sasa, AZ, ni wa kiwango kingine kabisa.
AZ Alkmaar wamekuwa katika kiwango cha juu na mchezaji wao, Troy Parrott, ambaye alifunga mabao manne katika mechi yao ya mwisho, amekuwa mchezaji wao tegemeo. Az wanatarajiwa kuwafunga PEC Zwolle kirahisi kama ambavyo wamefanya hivi karibuni dhidi ya Almere City, NEC, na RKC Waalwijk.
Changamoto nyingine itakayowakabili PEC Zwolle, ukiondoa udhaifu wa safu yao ya ulinzi na ubora wa safu ya ushambuliaji ya Az Alkmaar, ni uwepo wa rundo la majeruhi katika kikosi chao. PEC watalazimika kuingia katika mechi hii wakiwa wanawakosa wachezaji wao muhimu kama vile Braydon Manu, Samir Lagsir, na Tristan Gooijer.
Takwimu Muhimu:
*Katika mechi yao ya mwisho ya ligi, AZ walipata ushindi wa mabao 9-1 dhidi ya Heerenveen nyumbani, wakidumisha unbeaten yao msimu huu hadi mechi 5 (ushindi 4, sare 1), na sasa wapo katika nafasi ya pili na pointi 13, pointi mbili tu nyuma ya vinara PSV.
*PEC Zwolle kwa sasa wako katika nafasi ya 14 na pointi zao nne baada ya mechi tano. Katika mechi yao ya mwisho ya Eredivisie walicheza dhidi ya Twente na wakapata sare ya 1-1.
*Mara ya wa mwisho timu hizi kukutana katika Eredivisie ilikuwa katika msimu wa 2023/24 katika simba la AFAS Stadion matokeo yakiwa sare ya 2-2. Lennart Thy na Odysseus Velanas walifunga kwa upande wa Zwolle, wakati Vangelis Pavlidis na Sven Mijnans wakiifungia AZ.
Ubashiri wetu leo katika mechi hii Az Alkmaar kushinda
Angalia mkeka zaidi hapa chini
MATOKEO NDANI YA DAKIKA 90
⚽Nice - Saint-Etienne: 1 ✅
⚽Zwolle - AZ Alkmaar: 2 ✅
⚽Nacional - Sporting Braga: X2 ✅
⚽HB Koge - Vendsyssel: 2 ✅
⚽MTK - Ferencvaros: 2 ✅
JUU/CHINI [OVER/UNDER]
⚽Cagliari - Empoli: Under 3.5 ✅
⚽Augsburg - Mainz 05: Over 1.5 ✅
⚽Zwolle - AZ Alkmaar: Over 1.5 ✅
⚽Paderborn - Hannover 96: Over 1.5 ✅
⚽Schalke 04 - Darmstadt: Over 1.5 ✅
Post a Comment