Kombe la Shirikisho Afrika: Simba na Al Ahli Tripoli Watoka Sare ya 0-0


Simba SC ya Tanzania wamefanikiwa kulazimisha sare ya 0-0 na Al Ahli Tripoli ya Libya katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Juni 11 mjini Tripoli uliochezwa siku ya Jumapili, Septemba 15, 2024 (jana).


Mchezo huo ambao ulianza saa 10:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki ulishuhudia pande zote mbili zikipambana kwa bidii kutafuta ushindi muhimu kuelekea mchezo wa marudiano utakaofanyika wiki ijayo jijini Dar es Salaam, huku wenyeji wakionekana kufanya mashumbulizi zaidi. Hata hivyo, licha ya majaribio mengi kutoka pande zote, hakuna timu iliyoweza kupata bao katika mchezo huo.

Sare hii inamaanisha kuwa matumaini ya Simba ya kufuzu kwa hatua ya makundi bado yako hai, lakini watakuwa na changamoto kuwazuia wachezaji wa Al Ahli Tripoli ambao walionekana kuwa mwiba mkali katika mchezo huu wa kwanza.

Simba, ambao wameanza msimu wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wakiwa na kiwango bora, walifanikiwa kuwadhibiti Alhi kwa muda mrefu lakini walishindwa kutengeneza nafasi za wazi za kufunga. Al Ahly Tripoli, kwa upande mwingine, walitegemea mashambulizi ya haraka lakini walishindwa kuzitumia kwa ufanisi.

Mchezo wa marudiano kati ya timu hizi mbili unatarajiwa kuchezwa Septemba 22 katika dimba la Benjamin Mkapa ambapo Simba watatakiwa kupata ushindi au sare ya 0-0 ili kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Post a Comment

Previous Post Next Post