Lionel Messi Afikiria Kwenda Newell's Old Boys

 
Nyota wa soka wa Argentina, Lionel Messi, amezungumza kuhusu mipango yake ya baadaye baada ya mkataba wake na klabu ya Inter Miami kumalizika mwaka 2025.

Messi, mwenye umri wa miaka 37, alifanikiwa kushinda Copa America ya pili na Argentina mwaka huu. Hata hivyo, aliumia wakati wa fainali na kukosa mechi kadhaa za Inter Miami. Aliporudi alifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya mwisho ya goli katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Philadelphia Union.

Kulingana na ripoti kutoka Uhispania, Messi ameamua kurudi Argentina na kujiunga na klabu ya Newell's Old Boys, ambako alianza kazi yake ya soka, mara baada ya mkataba wake na Inter Miami kutamatika.

Messi anatarajia kujiunga na Newell's Old Boys mwezi Desemba 2025. Anaamini kwamba maamuzi ya kumalizia soka lake katika klabu hiyo itakuwa jambo la maana.

Messi mwenye umri wa miaka 37, bado anaendelea kuonyesha uwezo wake wa juu katika soka licha ya umri wake mkubwa. Amefunga mabao 14 na kutoa pasi za mwisho 10 katika mechi 15 za Inter Miami mwaka huu.

Post a Comment

Previous Post Next Post