Mkeka wa Leo 17 September 2024: Mpe Real Madrid Ushindi Dhidi ya VfB Stuttgart

 
Real Madrid wataanza utetezi wao wa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya VfB Stuttgart Jumanne usiku katika Uwanja wa Santiago Bernabeu. Hii ni mechi ya kwanza kabisa kuwahi kuzikutanisha timu hizi mbili na inatarajiwa kuwa rahisi kwa wenyeji ambao pia ni mabingwa watetezi wa taji hilo.

Real Madrid walichukua taji lao la kumi na tano la Ulaya msimu uliopita kwa ushindi dhidi ya Borussia Dortmund, wanatazamiwa kujitahidi kuanza kampeni yao kwa kishindo. Utawala wa Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa Ulaya sio suala la kutilia shaka hata kidogo, wamefanikiwa kubeba taji hilo mara sita katika muongo uliopita.

Stuttgart wao wanarudi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kutokuwepo kwa miaka 15, na wanatarajiwa kukutana na hali ngumu sana kwani katika hatua hii ya makundi, ukiondoa Real Madrid, pia wanatarajiwa kukutana na Juventus, Paris Saint-Germain na Atalanta!

Licha ya mafanikio yao ya hivi karibuni, Real Madrid wataingia katika mechi hiyo huku wachezaji wao muhimu ambao walizikosa mechi kadhaa kutokana na majeraha, Jude Bellingham na Aurelien Tchouameni wakirejea kikosini tayari kuwakabili Stuttgart.

Stuttgart, wenye wachezaji bora kama vile Ermedin Demirovic na Deniz Undav, watakuwa na wakati mgumu dhidi ya Madrid licha ya kwamba wametoka kupata matokeo dhidi ya Borussia Monchengladbach katika mchezo wa Bundesliga.

Mechi hiyo inatarajiwa kuwa ya ushindani mkali, lakini uzoefu na ubora wa Real Madrid utawapatia faida.

Takwimu Muhimu:

*Real Madrid hawajapoteza mechi hata moja katika michezo 13 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya

*Real Madrid wamefanikiwa kufunga goli angalau moja katika michezo 6 iliyopita

Ubashiri wetu leo katika mechi hii Real Madrid kushinda na Over 2.5

Angalia mkeka zaidi hapa chini

MATOKEO NDANI YA DAKIKA 90

⚽Bayern Munich - Dinamo Zagreb: 1 ✅

Real Madrid – Stuttgart: 1 

Brentford - Leyton Orient: 1 

Stoke City - Fleetwood Town: 1

Manchester United – Barnsley: 1 

Galatasaray - Gaziantep FK: 1 


JUU/CHINI [OVER/UNDER]

Young Boys - Aston Villa: Over 1.5 

Milan - Liverpool: Over 1.5 

Bayern Munich - Dinamo Zagreb: Over 2.5 

Real Madrid - Stuttgart: Over 2.5 

Brentford - Leyton Orient: Over 1.5 

Volendam - Dordrecht: Over 1.5 

Post a Comment

Previous Post Next Post