Kocha Mkuu wa Kengold Afikiria Kung’atuka

Fikiri Elias


Kocha mkuu wa Kengold FC, Fikiri Elias, anakabiliwa na shinikizo kubwa baada ya timu yake kupoteza mechi tatu mfululizo katika Ligi Kuu ya NBC. Matokeo mabaya ya ya hivi karibuni ni mechi ya jana Jumatatu dhidi ya KMC FC, ambapo goli la pekee la Redemtus Mussa mnamo dakika ya 16 ya mchezo lilitosha kuwafanya wageni hao wa ligi watoke uwanjani vichwa chini.

Baada ya mechi, Elias alitoa maneno yaliyoashiria uwezekano wa kujiuzulu nafasi yake. "Ninaamini kwamba malengo yangu hayajafikiwa baada ya raundi tatu za ligi," alisema. "Ninachukua hatua ya kukaa chini na uongozi wa klabu kujadili hatima yangu."

Msimu wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara 2024/25, ambao ni msimu wa kwanza kwa Kengold umeanza vibaya sana kwani hawajapata matokeo katika raundi 3 za mwanzo. Sio tu hawajashinda mechi zote tatu, lakini pia hawajapata hata sare na morali ya timu inaonekana kuwa chini.

Shinikizo kwa Elias lina uwezekano wa kuongezeka ikiwa Kengold wataendelea kufanya vibaya. Mashabiki wa klabu wanazidi kuwa na wasiwasi na wanahitaji matokeo. Uongozi wa klabu utahitaji kufanya uamuzi juu ya hatima ya Elias hivi karibuni.

Na Luck Mwaifuge

Post a Comment

Previous Post Next Post