Simba SC Yafuzu Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika

Klabu ya Simba imefanikiwa kufuzu rasmi hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho kwa msimu wa 2024-2025 baada ya ushindi wa kishindo wa 3-1 dhidi ya Al Ahli Tripoli kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Ushindi huu umewahakikishia Simba ushindi wa jumla wa 3-1, baada ya mechi ya kwanza kuisha kwa sare ya bila kufungana.


Simba SC ilianza mchezo kwa ari kubwa, ikitumia vyema faida ya kucheza nyumbani mbele ya mashabiki wao na kuonyesha mchezo wa kiwango cha juu. Uwanja wa Benjamin Mkapa ni machinjio ya Simba, na wachezaji hawajawaangusha mashabiki wao.

Magoli yaliyowapa heshima wababe hao wa Tanzania yalifungwa na Kibu Denis, Leonel Ateba na Edwin Balua. Kibu Denis, aliyeanza mechi kwa mara ya kwanza chini ya kocha Fadlu Davids, alifungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 36 akisawazisha goli la Ahli Tripoli lililofungwa na Mabululu. Goli la pili likiweka kambani na Leonel Ateba muda mfupi kabla ya mapumziko, akiweka mpira wavuni katika dakika ya 45+1. Edwin Balua, ambaye hakuwa ameanza mechi iliyopita, alifunga bao la tatu dakika ya 90, akihakikisha ushindi wa Simba.

Kocha Fadlu Davids alifanya mabadiliko kadhaa ya kimkakati kuelekea mchezo huu muhimu. Kibu Denis alipata nafasi ya kuanza, akichukua nafasi ya Edwin Balua, na alileta matokeo chanya kwa kufunga bao la kwanza katika kipindi cha kwanza. Safu ya kiungo na ulinzi ya Simba ilicheza kwa umakini mkubwa, ikiweza kuwazuia Al Ahly Tripoli wasipate nafasi ya kurudi mchezoni.

Post a Comment

Previous Post Next Post