Vinicius Jr Asikitishwa na Kiwango cha Brazil

Vinicius Jr wa Real Madrid ameonesha kusikitishwa na matokeo ya hivi karibuni ya Brazil katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia. Licha ya umahiri wake katika klabu ya Real Madrid, mshambuliaji huyo amekuwa akihangaika kuonesha kiwango hicho cha juu katika ngazi ya kimataifa.

Brazil kwa sasa wanashika nafasi ya tano katika msimamo wa CONMEBOL baada ya kupoteza 1-0 kwa Paraguay, wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kuhakikisha wanatinga moja kwa moja Kombe la Dunia la 2026. Vinicius Jr amewaomba msamaha mashabiki wakati akizungumzia kuhusu haja ya timu yake hiyo kuboresha aina yake ya uchezaji:

“Tunawaomba radhi mashabiki,ambao wako upande wetu wakati wote. Lakini tunahitaji kuwa bora zaidi... najua uwezo wangu, najua ninachoweza kufanya kwa timu yangu ya taifa. Umekuwa wakati mbaya kwa sababu kama huwezi kujiamini huwezi kufunga, kupiga pasi za mwisho wala kuonesha kiwango kizuri.”

“Tunajua hali tunayoipitia, tunataka kuiondoa Brazil katika hali hii kwa gharama yoyote ile, tunatakiwa kwenda nyumbani na kuanza kufikiria kuhusu kila tunachoweza kufanya ili tuanze kucheza vizuri tena. Hatuwezi kuwa tunakuja hapa, tunapoteza alama na kuendelea kucheza hivi. Ni kipindi kigumu, tunalazimika kupokea maoni na kila kukosolewa na kurudi mapema tuirudishe Brazil juu.”

Mshambuliaji huyo amekuwa akikosolewa kwa utendaji wake katika mechi za hivi karibuni za Brazil, lakini anaendelea kuwa na imani katika uwezo wake na wa timu kwa ujumla kurudi katika hali yake ya ubora.

Post a Comment

Previous Post Next Post