Ahmed Ally |
Sakata la timu hizi mbili kumgombea Kagoma lilianza mwishoni mwa dirisha hili kubwa la usajili likianzia na kile kilichotajwa kuwa mchezaji huyo alisaini timu zote mbili. Taarifa za awali zilidai kwamba Kagoma alishakubaliana kila kitu na Yanga, ikiwemo maslahi binafsi, ada ya uhamisho na kisha kusaini kabisa kabla badae hajaamua kusaini Simba kutokana na kile kilichotajwa kama ‘maslahi bora zaidi’, suala liliibua mgogoro mkubwa kati ya pande hizo tatu.
Uongozi wa Yanga, kupitia Afisa Habari wao ndugu Ally Kamwe ulimtaka Kagoma aiombe msamaha klabu ya Yanga kwa kitendo alichokifanya ili wao wamruhusu kuichezea timu yake ya Simba, kauli iliyopingwa vikali na mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji wa Mpira Tanzania, Mussa Kisoki akithibitisha kwamba Kagoma alifanya kila alichokifanya kwa maelekezo ya klabu iliyokua imimmiliki, yani Singida Fountain Gate, kwani hakuwa mchezaji huru hivyo hapaswi kuiomba msamaha klabu yoyote ile na kumtaka afanye hivyo ni kumdhalilisha.
Yusuph Kagoma |
Yanga tayari wamepeleka shauri hilo kwenye kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji na mpaka sasa yanasubiriwa maamuzi ya kamati hiyo kuhusu hatima ya Yusuph Kagoma.
Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa sakata hilo, afisa habari wa Simba, Ahmed Ally, amelizungumzia suala hilo akichapisha taarifa kwenye ukurusa wake wa mtandao wa Instagram akisema;
“Kwa mfano klabu yenu inampenda sana Yusuph Kagoma yaani kila mkilala mnamuota, roho zinawauma kumkosa na mnataka aje kwenu, Cha kufanya ni kuwa na subira,” ilisomeka sehemu ya ujumbe huo na kuongeza, “Kwa sasa Kagoma ana maika 23 na Isha Allah atakaa Simba kwa miaka 10+ akifikisha miaka 33 au 35 ndio atakuja kwenu”
Ujumbe wa Ahmed Ally uliendelea mbele zaidi ukisomeka, “Yaani mfumo ni ule ule kama mlivyomsubiri Mzambia kwa miaka 7 au mlivyomsubiri namba 20 kwa miaka 15, Kagoma nae ni hivyo hivyoo ila kwa sasa ni mali halali ya Simba.”
Post a Comment