Prince Dube Amalizana Rasmi na Azam FC

Katikati ni Prince Dube

Baada ya vuta nikuvute za tangu Machi mwaka huu hatimaye klabu ya Azam Fc imefikia makubaliano ya kuachana na aliyekuwa mchezaji wao kwa miaka minne Prince Dube.

“Tunapenda kuutaarifu umma kwamba tumeridhia maombi ya Prince Dube kuvunja mkataba wake nasi, aliyoyatoa Machi 2024”, ilisomeka sehemu ya taarifa rasmi ya klabu hiyo na kuongeza “ Hatua hii inafuatia kitendo cha mchezaji huyo kutimiza matakwa ya kimkataba kama ilivyoainishwa kwenye vipengele vinavyoruhusu upande mmoja kuvunja mkataba”

Ikumbukwe kwamba nyota huyo wa kimataifa wa Zimbabwe alijiunga na matajiri hao wa mitaa ya Chamazi mwaka 2020 akitokea The Highlanders ya nchini kwao Zimbabwe na amekuwa na wakati mzuri na wanachamazi hao licha ya kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

Prince Mpumelelo Dube aliwasilisha maombi ya kutaka kuachana na Azam mnamo mwezi wa tatu mwaka huu na timu hiyo kumtaka kutoa kiasi cha dola za kimarekani 300,000 kama takwa la kimkataba kati yao iwapo mwanamkataba mmoja atataka kuuvunja. Mpaka sasa ripoti zinaarifu kwamba nyota huyo amefanikiwa kulipa dola za kimarekani 200,000 hivyo kuruhusiwa kuachana na klabu hiyo baada ya majadiliano ya pande mbili.

Jiunge sasa Promocode ni 1029

Malipo hayo ya pesa yanasemekana kuwa yalifanyika siku ya Juni 29 na tayari wawakilishi wa mchezaji huyo wamewasilisha viambatanisho vya malipo hayo kwa uongozi wa Azam Fc.

Nyota huyo raia wa Zimbabwe aliye mapumzikoni nchini Ufaransa yupo tayari kutafuta changamoto mpya na tayari anahusishwa na mabingwa wa Ligu Kuu ya Soka Tanzania Bara, klabu ya Yanga Africa maarufu kama Wananchi ambao inasemekana ndio waliofanikisha zoezi zima la Prince Dube ‘Mgadafi’ kumalizana na Azam Fc na pia (Yanga) wanatajwa kuwa ndio wanaogharamia kila kitu kuhusu mapumziko ya nyota huyo nchini Ufaransa.

Itoshe kusema kuwa Prince Mpumelelo Dube si mchezaji wa Azam Fc tena na kinachosubiriwa ni muda tu kabla hajatambulishwa rasmi mitaa ya Twiga na Jangwani kwenda kuungana na wakaliwakali wengine kama Stephan Aziz Ki, Pacome Zouzou na Maxi Nzengeli.

Na Luck Mwaifuge

Post a Comment

Previous Post Next Post