Mkwaju wa penati uliopigwa na Christiano Ronaldo katika kipindi cha kwanza cha dakika 30 za nyongeza za mechi ya hatua ya 16 bora kati ya Ureno na Slovenia uliokolewa na golikipa Jan Oblak na kumfanya Ronaldo abubujikwe na machozi kwa kushindwa kuipa uongozi timu yake hiyo.
Cristiano Ronaldo akiangua Kilio baada ya kukosa Mkwaju wa Penati |
Dakika 90 za mechi hiyo zilimalizika kwa sare ya bila kufungana hivyo kulazimika kuendelea kwa dakika 30 zaidi kabla ya kuja kuamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati.
Nahodha huyo wa Ureno, alichukua jukumu la kupiga penati hiyo muhimu iliyopatikana katika kipindi cha kwanza cha dakika za nyongeza lakini jaribio hilo lilizimwa na Jan Oblak aliefanikiwa kuupangulia mpira huo kwenye nguzo ya upande wa kushoto na kumuacha Ronaldo haamini kilichotokea.
Mama yake Ronaldo akimwaga Chozi Baada ya Mwanae Kukosa Mkwaju wa Penati |
Sio tu Ronaldo, hata mashabiki wa Ureno waliamini kwamba penati ile ingemaliza mchezo hivyo matarajio hayo yalimfanya adondeshe chozi kwa hisia kali akiamini ameshindwa kuivusha timu yake kwenda hatua inayofuata.
Licha ya Ronaldo kupiga mashuti zaidi ya 8 kutafuta goli aivushe timu yake kwenda hatua inayofuata lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda na mechi hiyo ikatamatika kwa sare ya bila kufungana sio tu katika dakika 90 bali hata zile 30 za ziada hivyo kuamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati.
Usiku wa mechi hii hautosahaulika kirahisi na Christian Ronaldo kwani ulikuwa na mchanganyiko wa hisia kwa nyota huyo ukianzia kuwa wenye huzuni sana na kuishia kuwa wa furaha kubwa.
Baada ya kukata tamaa, na wapenzi wa soka duniani kote kuamini kwamba lolote linaweza kutokea katika changamoto ya mikwaju ya penati ikiwemo hata Slovenia kwenda hatua ya Robo Fainali kwani kama wanavyosema penati hazina mwenyewe, Ronaldo anakua mchezaji wa kwanza kupiga penati kwa timu yake na kuifungia goli la kwanza, mbili nyingine zikifungwa na Bruno Fernandez na Bernardo Silva huku kipa Diogo Costa (Ureno) akiokoa penati za Josip Illicic, Jure Balkovec na Benjamin Verbic.
Matokeo hayo yanawafanya Ureno wafuzu kwenda hatua inayofuata ya Robo Fainali wakiwafuata Ufaransa ambao wao waliwatoa Ubelgiji kwa ushindi wa goli 1 kwa bila. Mechi hii ya Robo Fainali itapigwa tarehe 5 Ijumaa.

Na Luck Mwaifuge
Post a Comment