Euro 2024: Spalletti Bado Yupo yupo Italia

Licha ya kuondoshwa mashindanoni katika hatua ya 16 bora, mabingwa watetezi wa Euro, Italia, wataendelea kufundishwa na kocha Luciano Spalletti. Uamuzi huo unakuja baada ya minong'ono iliyokuwepo kwa mashabiki mbalimbali wa Italia kuhusu hatima na kocha huyo ndani ya kikosi cha Italia baada ya kupokea kichapo cha 2-0 kutoka kwa Switzerland.

Luciano Spalletti
Hayo yaliwekwa wazi na raisi wa chama cha soka Italia, Gabriele Gavrina katika mkutano wake na waandishi wa habari siku ya Jumapili. “Bado tuna imani na Spalletti na tutaendelea nae. Haiyumkiniki kubadilisha kocha mkuu na kuuacha huu mradi”, alisema.

Italia walifanikiwa kujikusanyia alama 4 kwenye Kundi B huku wakimaliza nafasi ya pili nyuma ya vinara Hispania waliomaliza na alama 9 huku wakishinda mchezo mmoja, sare mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja.

Kibarua cha Spalletti kilikua mashakani licha ya kuwa ameiongoza timu hiyo katika michezo 14 tu huku akishinda michezo 7, sare mara 4 na kupoteza mara 3 huku vipigo viwili kati ya hivyo vikiwa ni katika mashindano ya Euro msimu huu ikiwa ni pamoja na kile cha 1-0 kutoka kwa Hispania, na 2-0 kutoka kwa Switzerland.

Akiwa na mkataba na mabingwa hao wa Euro 2020, Spalletti sasa mipango yake yote ni kuhusu mashindano yajayo ya Kombe la Dunia yatakayofanyika Amerika ya Kusini. Hata hivyo anakiri kwamba timu yake itahitaji maboresho. “Sijakuwa bora” anakiri, “kiwango chetu dhidi ya Switzerland hakikuwa cha kuridhisha. Lakini ninao mpango. Tunahitaji kuwa na kikosi chenye vijana, timu hii inatakiwa kurekebishwa kuanzia chini kabisa”

Kikosi cha Italia kilichoitwa kwa ajiri ya mashindano haya ha Euro 2024 kiliundwa na wachezaji kama vile Giovanni Di Lorenzo (30), Matteo Darmian (34), Gianluca Mancini (28), Jorginho (32), Bryan Cristante (28), Stephan el Shaarawry (31) na wengineo wengi na sasa Spalletti anafikiria kupunguza wachezaji wenye umri mkubwa ndio suluhisho.

Na Luck Mwaifuge

Post a Comment

Previous Post Next Post