Bodi ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara (TPLB) leo Ijumaa, tarehe 5 Julai imetangaza rasmi tarehe ya kuanza kwa msimu mpya wa 2024/2025 ambapo ligi hiyo itaanza tarehe 17 mwezi wa 8 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Bodi ya ligi, Almas Kasongo, ligi hiyo inatarajiwa kumalizika mwezi wa 6 mwaka 2025.
CEO wa Ligi Kuu Tanzania Bara Bw. Almas Kasongo |
"Ligi Kuu ya NBC itaanza katikati ya mwezi wa 8 (tarehe 17), baada ya Ngao ya Hisani, Mipango bado inaendelea.” Alisema Kasongo akiongea na waandishi wa habari.
Hata hivyo Kasongo amebainisha kwamba ratiba ya Ligi hiyo inaweza kuwa na mabadiliko wakati wowote kulingana na ratiba mbalimbali za michezo ya FIFA NA CAF hivyo kuzitaka timu zote ziwe tayari kuendana na mabadiliko hayo.
Pamoja na hilo, Almas Kasongo akijibu swali la mwandishi mmoja aliyeuliza iwapo VAR kuanza kutumika katika ligi kutatatua changamoto ya makosa ya waamuzi ambapo amesema, “Pamoja na kuja kuwa na VAR kwenye Ligi Kuu ya NBC sioni ikimaliza kabisa changamoto za maamuzi kwenye michezo yetu.”
Na Luck Mwaifuge
Post a Comment