Kiungo wa Manchester United, Marcus Rashford, amejikuta na wakati mgumu baada ya mahakama kumuadhibu kwa kosa la kuendesha gari kwa uzembe.
Marcus Rashford |
Rashford anadaiwa kuendesha gari lake
aina ya Rolls Royce kwa mwendokasi kupitiliza hadi kufikia kwenda maili 104 kwa
saa kwenye barabara kuu ya M60 akitoka kwenye kumbi za starehe. Adhabu
alizopewa nyota huyo wa Manchester United ni: marufuku ya kuendesha gari kwa
miezi sita, faini ya pauni £1,666, na gari lake hilo la kifahari lenye
thamani ya £560,000 kuwekwa kizuizini.
Hii sio mara ya kwanza kwa Rashford
kupata matatizo barabarani. Miezi michache tu iliyopita, alihusika kwenye ajali
akiwa na mojawapo ya magari yake mengine ya kifahari.
Ripoti zinasema katika utetezi wake
Rashford alidai alihisi anafuatiliwa, ndio maana aliendesha kwa mwendo kasi.
Hata hivyo, mamlaka hazikuridhika na sababu zake.
Wakati huu ikiwa msimu mpya unakaribia
kuanza, Rashford atalazimika kuachana na kiti cha dereva na kukaa upande wa
abiria, akitegemea wachezaji wenzake au usafiri mbadala hadi adhabu yake yake
itakapomalizika. Maswali ni mengi, Je sakata hili litaathiri uwezo wake
uwanjani? ni wakati pekee ndio utaweza kutuambia ukweli, lakini jambo moja ni
hakika: Rashford atalazimika kuzingatia namna yake ya uendeshaji hususani
katika barabara za umma.
Tukio hili linatumika kama tahadhari kwa wachezaji wa mpira na mashabiki pia wenye tabia kama za mchezaji huyo. Ingawa inaweza kuonekana kwamba magari ya kifahari na mwendo kasi ni vitu vinavyoenda sambamba, kuzingatia sheria ni muhimu ili kuepuka sio tu faini au kufungiwa kuendesha, lakini pia hata ajali zinazoweza kuepukika. Pengine Rashford anaweza kutumia muda huu kuboresha ujuzi wake wa kupiga pasi - uwanjani, bila shaka!
Post a Comment