Klabu ya Yanga SC imezindua rasmi jezi zake mpya kwa ajili ya msimu wa 2024/2025. Jezi hizi zimebuniwa kwa ubunifu wa hali ya juu na zinaonekana kuvutia mashabiki wengi. Jezi hizi mpya zimeanza kupatikana katika maduka mbalimbali kwa bei ya TSh 45,000/=
Jezi
za Nyumbani (Home Kit) Jezi ya nyumbani ya Yanga SC
kwa msimu wa 2024/2025 imebuniwa kwa rangi ya kijani na michoro ya dhahabu.
Inaonekana ya kuvutia na inawakilisha vizuri klabu hii yenye historia kubwa
katika soka la Tanzania. Rangi ya kijani ni alama ya ujasiri na nguvu ya timu,
wakati michoro ya dhahabu inaashiria mafanikio.
Jezi
za Ugenini (Away Kit): Jezi za ugenini za Yanga SC
zimebuniwa kwa rangi ya manjano na bluu, zikiwa na michoro inayovutia. Rangi ya
manjano inaashiria matumaini, huku bluu ikiwa ni alama ya utulivu na imani.
Jezi
ya Tatu ya Yanga (Third Kit) Yanga SC imezindua jezi
za tatu ambazo zimebuniwa kwa rangi ya nyeusi na michoro ya kijivu. Jezi hizi
zina muonekano wa kipekee na zinawakilisha mtindo wa kisasa. Rangi ya nyeusi
inaashiria nguvu na uthabiti.
Mashabiki wa Yanga SC wanaweza kupata
jezi hizi mpya katika maduka rasmi ya klabu na maduka mengine yanayouza vifaa
vya michezo kwa bei ya shilingi 45,000.
Post a Comment