England imejipanga kuendelea na mfululizo wao wa kutopoteza dhidi ya Finland wakati timu hizo mbili zitakapomenyana katika Uwanja wa Wembley katika mchezo wao wa Kundi B2 la UEFA Nations League. England bado wana ari ya ushindi wakichochewa na ushindi wa 2-0 dhidi ya Jamhuri ya Ireland katika mchezo wao wa kwanza, wanatarajiwa kudumisha utawala wao dhidi ya Finland.
Safu ya ulinzi ya England, ikiongozwa na wakali Marc Guehi na Harry Maguire, walionekana kuwa wenye nidhamu na ubora katika mchezo wao wa mwisho. Uwezo wao wa kupunguza nafasi za wapinzani wao umekuwa sifa ya mafanikio yao ya hivi karibuni, na watakuwa kuhakikisha wanaisaidia timu yao kutoruhusu mashambulizi ya Finland kumfikia golikipa wao.
Katika eneo la ushambuliaji, England ina wachezaji wenye vipaji wa daraja la juu kabisa ikiwa ni pamoja na Harry Kane, Bukayo Saka, na Jack Grealish. Ubunifu wao na uwezo wao wa kufunga huwapa wapinzani wao kazi ya ziada kuwazuia, nyota hao wanatarajiwa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga dhidi ya safu ya ulinzi isiyo imara sana ya Finland
Finland, kwa upande mwingine, wanaingia katika mchezo huu wakiwa wametoka kupokea kipigo cha 3-0 dhidi ya Ugiriki, mechi iyoonesha ubovu wa safu yao ya ulinzi lakini pia ubutu wa ile ya ushambuliaji.
Kihistoria, England imetawala katika mechi zilizowakutanisha na Finland, ikishinda mechi 5 na kupata sare 2 katika mechi zao 7 zilizopita. England wamekuwa na muendelezo mzuri dhidi ya wapinzani wao hawa na wanatarajiwa kuendelea na mwenendo huo katika mchezo huu.
Kwa kuzingatia uwezo imara wa England, faida ya uwanja wa nyumbani, na namna walivyotawala mechi zilizowakutanishana Finland, ni vigumu kuona kitu kingine chochote zaidi ya ushindi rahisi kwa England katika mchezo huu.
Takwimu Muhimu:
*England wamepoteza mchezo mmoja tu kati ya michezo yao minane iliyopita.
*England imeshinda michezo yote (3) dhidi ya Finland katika uwanja wa Wembley, pia magoli zaidi ya 2.5 yalifungwa.
*Finland wamefungwa mabao tisa katika michezo yao mitatu iliyopita, wao wakifunga manne.
Ubashiri wetu leo katika mechi hii England kushinda na Over 2.5.
Angalia mkeka zaidi hapa chini
MATOKEO NDANI YA DAKIKA 90
⚽Hungary – Bosnia: 1X ✅
⚽Indonesia – Australia: 2 ❌
⚽England – Finland: 1 ✅
⚽Bahrain – Japan: 2 ✅
⚽Botswana – Egypt: 2 ✅
⚽South Sudan - South Africa: 2 ✅
JUU/CHINI [OVER/UNDER]
⚽Netherlands – Germany: Over 1.5 ✅
⚽England – Finland: Over 2.5 ❌
⚽Bahrain – Japan: Over 1.5 ✅
⚽Wrexham - Salford City: Over 1.5 ✅
Post a Comment