Meneja wa Arsenal Mikel Arteta alisema "alishangazwa" kuona Declan Rice akitolewa kwa kadi nyekundu katika sare ya 1-1 dhidi ya Brighton baada ya "kutofautiana" na mwamuzi Chris Kavanagh.
Akiwa tayari amepewa kadi ya njano kwa kumchezea vibaya Joel Veltman wa Brighton, kiungo wa kati wa Uingereza Rice alipokea kadi ya pili ya njano dakika nne za kipindi cha pili kwa kuupiga mpira nje beki huyo wa Uholanzi akijaribu kupiga mpira wa adhabu.
Dakika tisa baadaye Joao Pedro alisawazisha bao la kuongoza la Kai Havertz kuendeleza rekodi ya Brighton mwanzoni mwa msimu bila kufungwa na kuhitimisha rekodi ya Arsenal ya ushindi 100%.
"Nilishangaa," Arteta alisema. "Kushangaa, kushangaa, kushangaa kwa sababu ya jinsi maamuzi yanaweza kutofautiana. Katika kipindi cha kwanza, kuna matukio mawili na hakuna kinachotokea.
"Kisha, kwenye eneo lisilo la muhimu, mpira unamgonga Declan [nyuma ya mguu wake], anageuka, haoni mchezaji anakuja na anagusa mpira. "Kwa mujibu wa sheria, anaweza kuchukua maamuzi hayo, lakini kwa mujibu wa sheria anahitaji kufanya uamuzi unaofuata, ambayo ni kadi nyekundu ili tucheze 10 kwa 10. Hili ndilo lililonishangaza. Katika kiwango hiki ni cha kushangaza."
Mechi hiyo iligeuka na kuwapendelea Brighton baada ya Arsenal kushuka hadi wachezaji 10 na Seagulls wakapiga mashuti 19 kwa matatu na idadi ya mabao iliyotarajiwa kuwa 1.9.
Arteta aliamini timu yake "ilistahili kushinda mchezo" na kwamba mshambulianji wa Brighton Pedro angepewa kadi ya njano kwa kuupiga mpira nje mara tu filimbi ilipoanza kipindi cha kwanza.
Lakini bosi mgeni Fabian Hurzeler alisema huwezi kulinganisha matukio na Rice alistahili kutolewa. "Kwangu mimi, kadi nyekundu ni ya wazi," aliongeza. "Anapiga mpira nje, ni kupoteza muda. "Huwezi kulinganisha hali hizi mbili. Ya kwanza na Joao ni wazi kuwa ni mpira wa adhabu na hali tuli. Nyingine ni kama hali ya mabadiliko. "Tafadhali usilinganishe hali hizi, kwa sababu katika soka hali mbili hazifanani kwa hivyo hatuwezi kulinganisha hali hizi."
Ni hasa kilichotokea?
Rice, aliyepewa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza kwa kumchezea vibaya Veltman, aliadhibiwa kwa kumzonga mchezaji huyo huyo ndani ya nusu ya Brighton karibu na mstari wa kugusa.
Veltman aliporudi kwa miguu yake, mlinzi wa Albion alikwenda kuchukua mpira wa adhabu kwa haraka na kuusogeza mbele lakini, alipojaribu kufanya hivyo, Rice aliuondoa mpira huo.
Veltman aliendelea na ufuatiliaji wake, akimpiga teke mchezaji wa Gunners na kumpeleka chini.
Wakati seti zote mbili za wachezaji zikiwa zimemzonga mwamuzi, mashabiki wa Arsenal ndani ya Uwanja wa Emirates walikuwa wakitaka Veltman aonyeshwe kadi - na kukawa na miguno wakati Rice ndiye aliyetolewa nje kwa kadi nyekundu. Kiungo huyo wa kati wa Uingereza alionekana kupigwa na butwaa.
Sheria zinasemaje?
Ligi ya Uingereza ilithibitisha kwamba Rice alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwa "kuchelewesha kuanza tena kwa mchezo" - na, kwa mujibu wa sheria ya 12 kwenye tovuti ya Chama cha Soka, hili ni kosa linalostahili onyo.
Hii ni pamoja na "kupiga teke au kubeba mpira mbali, au kuzua makabiliano kwa kugusa mpira kimakusudi baada ya mwamuzi kusimamisha mchezo".
Mwamuzi wa zamani Mike Dean alisema iliwekwa wazi kwa timu kabla ya msimu kuanza kwamba kuupiga mpira nje kunaweza kusababisha kupelekea kupta kadi.
"Kwa bahati mbaya kwa Declan alipiga mpira nje," Dean alisema kwenye Sky Sports. "Hakuupiga mbali, lakini waliambiwa kabla ya msimu, piga mpira uende mbali, chelewesha aina yoyote ya kuanza tena utaonywa, tayari alikuwa na kadi ya njano na hakuwa na jinsi zaidi ya kumtoa nje.
"Alichelewesha kuanza tena kwa sababu Brighton walitaka kuanzisha mpira haraka uwanjani."
Lakini beki wa zamani wa Arsenal Martin Keown alihisi kuwa ulikuwa uamuzi mbaya. "Ninajua kwamba Declan alipiga mpira mbali, lakini kwa nini Veltman anapiga mpira kwenye njia ya Rice?" Alisema kwenye TNT Sports.
"Ninajua kanuni ya sheria hii mpya, lakini mwamuzi ana jukumu la kuhakikisha seti zote mbili za wachezaji 11 uwanjani - sihisi kama ni kosa la kutolewa nje."
Beki wa pembeni wa zamani wa Liverpool Stephen Warnock alihisi kuwa Rice alimlazimisha mwamuzi kufanya uamuzi. "Declan Rice anajua anachofanya," Warnock alisema kwenye kipindi cha Matokeo ya Mwisho cha BBC.
"Ameangalia kidogo na kuupiga mpira mbali, kisha changamoto inaingia. "Unamwomba mwamuzi atoe uamuzi katika uamuzi huo. Unapozuia mpira katika nafasi hiyo kwa nini ufanye hivyo?"
Post a Comment