Haji Mnoga |
Beki wa kimataifa wa Tanzania Haji Mnoga amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Salford City, timu inayoshiriki Ligi daraja la nne la Uingereza. Mnoga anajiunga na Salford kutoka Portsmouth, ambapo amekuwa akicheza kwa muda mrefu.
Mnoga amesaini mkataba wa mwaka mmoja na Salford City, wenye kipengele cha kuongezwa ikiwa ataonyesha kiwango bora. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amesema anafurahia fursa ya kucheza Salford na anaamini itamsaidia kupandisha kiwango chake.
“Najisikia vizuri sana. Nina furaha kuona hili limekamilika sasa na nina hamu sana ya kuanza kuitumikia klabu hii.” Mnoga alisema.
Mnoga kabla ya kujiunga na Slaford alichezea Gillingham kwa mkopo kutoka Portsmouth. Beki huyo anajulikana kwa kasi yake, nguvu, na ujuzi wake wa ulinzi wa kuzuia.
Kocha wa Salford City Neil Wood amesema anafurahia fursa ya kufanya kazi na Mnoga. “Ni beki mwenye kipaji na ana uwezo mkubwa,” Wood alisema. “Ninatarajia kumwona akionesha kiwango kikubwa na Salford City.”
Usajili wa Mnoga ni moja kati ya jitihada za Salford City katika kutaka kupanda ngazi za soka la Uingereza. Klabu hiyo ina malengo ya kufikia Premier League na kujiunga kwa Mnoga kunaweza kuwapa msaada kufikia malengo yao.
Post a Comment