Mwinyi Zahera |
Klabu ya soka ya Namungo FC inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC imeachana na kocha wao mkuu Mwinyi Zahera. Baada ya mwanzo mbaya wa msimu, klabu hiyo imefikia uamuzi wa kumfuta kazi Mwinyi Zahera na tetesi ni kwamba ipo katika mazungumzo na kocha wa Simba Queens, Juma Mgunda, ili kuweza kuchukua nafasi hiyo.
Kibarua cha Zahera katika klabu ya Namungo kimekuwa cha muda mfupi kwani alijiunga na klabu hiyo Desemba 30, 2023. Katika mechi zake 19 alizoiongoza Namungo ameisaidia timu hiyo kushinda mechi 4 tu, huku akipata sare 7 na kupoteza mechi 8.
Ikiwa Ligi Kuu ya NBC imechezwa kwa mizunguko miwili tu, Zahera anakuwa kocha wa tatu kufutwa kazi akitanguliwa na David Ouma aliyekua Coastal Union na Youssouf Dabo wa Azam FC. Mabadiliko haya ya makocha yanaonyesha namna ambavyo timu hizi za ligi kuu zinashinikiza kupata matokeo mazuri kulingana na aina ya uwekezaji walioufanya na malengo waliyojiwekea.
Namungo FC sasa wanamfukuzia Juma Mgunda, kocha mwenye heshima kubwa katika soka la Tanzania, ili kuziba nafasi hiyo iliyo wazi. Iwapo watafanikiwa kumpata kocha huyo wanatazamiwa kupata matokeo chanya na mtazamo mpya kwenye timu hiyo.
Post a Comment