Mateo Kovacic anafikiria uwezekano wa kuondoka Manchester City mwezi Januari, na Saudi Arabia ikionekana kuwa sehemu anapoweza kutimkia. Mustakabali wa kiungo huyo wa Croatia pale Etihad umekuwa na mashaka tangu kuwasili kwa Ilkay Gundogan.
Kurudi kwa Gundogan pale City katika dirisha la usajili la kiangazi kumeleta wasiwasi kwa Kovacic kuhusu muda wake wa kucheza. Licha ya kuwa mchezaji muhimu katika mafanikio ya timu mwanzoni mwa msimu, kiungo huyo anaogopa kwamba nafasi yake inaweza kuchukuliwa na Gundogan na yeye asipate muda mwingi wa kucheza.
Al-Nassr, klabu ya Saudi Arabia iliyo na wachezaji kama Cristiano Ronaldo na Sadio Mane imetangaza nia ya kumsaini Kovacic. Wanaripotiwa kuwa tayari kutoa mkataba wa kuvutia wenye thamani ya takriban $65 milioni.
Suala la iwapo Manchester City wataruhusu kuondoka kwa Kovacic mwezi Januari bado ni kitendawili, lakini uamuzi wa kiungo huyo utategemea na iwapo watakua tayari kumpa muda wa kutosha kiwanjani ili asivutiwe na ofa ya Al Nassr.
Post a Comment