Kuelekea Jumapili: Simba Watembelea Kituo cha Kulelea Watoto Yatima ‘Hiyari’

Wababe wa soka la Tanzania, Simba SC, wameeneza furaha na umoja katika Kituo cha kulelea watoto yatima cha Hiyari Kabla ya Mchezo wao CAFCC dhidi ya Al Ahli Tripoli siku ya Jumapili Septemba 22, 2024.

Ahmed Ally katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto katika kituo cha 
kutunza watoto yatima cha Hiyari

Simba SC walifanya ziara katika kituo hicho cha watoto yatima cha Hiyari kama sehemu ya maandalizi yao ya mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho la Soka barani Afrika (CAFCC) dhidi ya Al Ahli Tripoli. Ziara hiyo ilikuwa ni namna ya kujitolea kwa klabu hiyo na uwajibikaji wa kurudisha kwa kijamii.

Uwepo wa sehemu ya uongozi wa timu hiyo ulileta furaha na msisimko mkubwa kwa watoto katika kituo hicho cha Hiyari. Msafara wa klabu, ukiongozwa na Afisa Habari Ahmed Ally na mashabiki wa timu walishiriki michezo mbalimbali na watoto na kugawa zawadi mbalimbali. Klabu hiyo pia ilitoa chakula cha mchana kwa watoto hao, kwa hisani ya MeTL Group, mdhamini wa klabu.

Na Luck Mwaifuge

Post a Comment

Previous Post Next Post