Manchester United wanaripotiwa kumfuatilia Peio Canales, kiungo wa kati kutoka Athletic Bilbao. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 amekuwa akitamba kwenye La Liga na anatarajiwa kuwa nyota mkubwa hapo baadae.
Canales ni zao la academy maarufu ya vijana ya Athletic Bilbao, ambayo imetoa vipaji kadhaa miaka ya hivi karibuni. Wachezaji mashuhuri kama Nico Williams na Iñaki Williams ni mazao ya kituo hicho cha kukuzia vipaji na hivi sasa wana mafanikio makubwa katika soka.
Nia ya United kwa Canales inawiana na mkakati wao wa kuwekeza kwa wachezaji wenye umri mdogo na vipaji vikubwa. Msimu huu wa majira ya joto, walifanikiwa kuinasa saini ya kiungo wa kati wa Mali Sekou Kone, mchezaji mwingine mwenye matarajio makubwa.
Kwa mujibu wa ripoti, Mashetani Wekundu wamekuwa wakifuatilia kwa karibu maendeleo ya Canales na kuna uwezekano wa kuendelea kufanya hivyo katika miezi ijayo. Ingawa anachezea Athletic Club B, uchezaji wake umevutia vilabu kadhaa, ikiwa ni pamoja na Manchester United.
Mkataba wa Canales na Athletic Club utaendelea hadi 2027, lakini fursa ya kujiunga na klabu kubwa kama Manchester United na uwezekano wa kufuata nyayo za wachezaji kama Kobbie Mainoo na Alejandro Garnacho inaweza kuwa kivutio kwa kinda huyo.
United itakabiliwa na ushindani kutoka kwa vilabu vingine vinavyovutiwa na Canales. Kipaji na uwezo wa kijana huyo umevutia timu kadhaa za Ulaya, na kumfanya kuwa mchezaji anayewindwa sana sokoni.
Na Luck Mwaifuge
Post a Comment