Salford City watatafuta ushindi wao wa kwanza msimu huu watakapowakaribisha MK Dons kwenye Uwanja wa Peninsula Jumatatu katika mchezo wa Ligi. Timu zote mbili zimeanza msimu kwa matokeo tofauti, lakini MK Dons angalau wamepata ushindi hivi karibuni dhidi ya Carlisle United.
Salford City wamekuwa na mwanzo mgumu wa msimu wakipoteza mechi tano na kutoka sare mbili katika mechi zao za ushindani. Wamekuwa dhaifu sana nyumbani, wakipoteza mechi tatu mfululizo kwenye Uwanja wa Peninsula. Hata hivyo, bao la dakika za mwisho katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Chesterfield liliwasaidia kupata sare hivyo kuinua matumaini ya kufanya vizuri katika michezo ijayo.
MK Dons, kwa upande mwingine, angalau wameonyesha ishara nzuri baada ya mwanzo mbaya katika Ligi kwani walipata ushindi mnono wa 3-0 dhidi ya Carlisle United uliovunja mfululizo wao wa mechi saba bila kushinda.
Salford watalazimika kuwakabili MK Dons bila beki Curtis Tilt kutokana na kusimamishwa, wakati Matthew Lund na Ryan Watson wanatarajiwa kurejea kutoka kikosini mara baada ya kupona majeraha yaliyowafanya wakose mechi kadhaa. Salford City, maarufu kama ‘The Ammies’ pia wamefanya sajili kadhaa siku ya mwisho wa dirisha la uhamisho, ikiwa ni pamoja na kuwaongeza kikosini Hakeem Adelakun, Frankie Okoronkwo, Kylian Kouassi, na Haji Mnoga.
Kwa upande wa MK Dons wao watawakosa Matt Dennis na Jonathan Leko kutokana na majeraha wakati Liam Kelly anatarajiwa kurejea kwenye kikosi baada ya kukosa mechi tatu na anaweza kuanza dhidi ya Salford.
Licha ya faida ya kuchezea uwanja wa nyumbani kwa Salford bado MK Dons wanatarajiwa kushinda mchezo huu kutokana na ubora wao wa hivi karibuni na namna ambavyo wamekuwa wakishinda mechi zao dhidi ya Salford.
Takwimu Muhimu:
💡Salford City hawajashinda mchezo wowote katika mechi mbili za mwisho zilizowakutanisha na Milton Keynes Dons
💡Katika mechi hizo mbili, Salford City wamefanikiwa kufunga magoli matatu tu huku wakiruhusu magoli 7.
Ubashiri wetu leo katika mechi hii MK Dons Kushinda.
Angalia mkeka zaidi hapa chini
MATOKEO NDANI YA DAKIKA 90
⚽Hfx Wanderers FC – York United X2 ❌
⚽Hobro – B 93 Copenhagen 1 ❌
⚽Salford City – MK Dons 2 ❌
⚽Ascoli – Pianese 1 ✅
⚽Raufoss – Sogndal 2 ❌
JUU/CHINI [OVER/UNDER]
⚽Jonkopings Södra – Norrby IF Over 1.5 ❌
⚽Trollhattan – Ljungskile SK Over1.5 ✅
⚽Eibar – Levante Over 1.5 ✅
⚽Elche – Cordoba Under 3.5 ❌
⚽Universitatea Cluj – Dinamo Bucharest Under 3.5 ✅
Post a Comment