Leo Alhamisi, Tottenham Hotspur wataanza kampeni yao ya Ligi ya Europa kwa mechi dhidi ya mabingwa wa Azerbaijan, Qarabag FK. Kikosi cha Ange Postecoglou, ambacho kwa sasa kiko katikati ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza, kimeonesha ufanisi licha ya kupoteza hivi karibuni dhidi ya Arsenal na Newcastle.
Wakati Postecoglou anatarajiwa kufanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi chake kwenye michi hii kutokana na kukabiliwa na mechi muhimu ya Ligi Kuu dhidi ya Manchester United, Spurs bado wanatarajiwa kutawala mechi hii.
Wachezaji muhimu kama Son Heung-min na James Maddison wataweza kupumzishwa, lakini nyota mpya Dominic Solanke anaweza kupewa nafasi ili kuendelea kujenga hali ya kujiamini.
Qarabag wao wanaingia kwenye mechi hii wakiwa na hali nzuri baada ya kushinda mechi tatu mfululizo na kuongoza ligi ya Azerbaijan. Hata hivyo, rekodi yao dhidi ya timu za Uingereza ni mbaya, wakiwa wamepoteza mechi zote sita walizokutana nazo, ikiwemo mechi mbili dhidi ya Spurs mwaka 2015.
Safari ya Qarabag katika mashindano ya Ulaya msimu uliopita ilimalizika katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Europa, lakini wanatarajia kufanya vizuri na kuanza vyema hatua ya makundi.
Licha ya maendeleo na matarajio hayo ya Qarabag, Tottenham wanatarajiwa kushinda kwa urahisi. Wakiwa na faida ya kucheza nyumbani na kikosi chenye uwezo mkubwa, Spurs wanapaswa kuwa na nguvu za kutosha kupata matokeo mazuri na kuanza vyema kampeni yao ya Ligi ya Europa.
Takwimu Muhimu:
*Timu hizi mbili zimekutana mara mbili, mara zote ikiwa katika hatua ya makundi ya Ligi ya Europa msimu wa 2015-16, ambapo Tottenham walishinda mechi zote mbili.
*Spurs wamepoteza mechi moja tu kati ya mechi zao nane za mwisho katika Ligi ya Europa, wakifunga angalau mabao matatu katika mechi tano.
*Tottenham wako kwenye mfululizo wa ushindi wa mechi sita nyumbani katika mashindano haya, huku wakiwa hawajaruhusu nyavu zao kuguswa katika mechi tano mfululizo.
*Qarabag wameshinda moja tu kati ya mechi zao nne za ugenini kwenye mashindano haya, wakifunga mabao 8 na kuruhusu mabao 12.
*Qarabag wamepoteza mechi zote sita walizokutana na timu za Kiingereza kwenye mashindano ya Ulaya, wakifunga mara moja na kuruhusu mabao 18.
Ubashiri wetu leo katika mechi hii ni Tottenham Hotspur Kushinda
Angalia mkeka zaidi hapa chini
MATOKEO NDANI YA DAKIKA 90
⚽Fenerbahce - Union Saint-Gilloise: 1
⚽Tottenham - Qarabag: 1
⚽Eintracht Frankfurt - Viktoria Plzen: 1
⚽Napoli - Palermo: 1
⚽Avarta - Esbjerg: 2
⚽HB Koge - FC Copenhagen: 2
JUU/CHINI [OVER/UNDER]
⚽Tottenham - Qarabag: Over 2.5
⚽Ajax - Besiktas: Over 1.5
⚽Eintracht Frankfurt -Viktoria Plzen: Over 1.5
⚽Cercle Brugge - Gent: Over 1.5
⚽HB Koge - FC Copenhagen: Over 1.5

Post a Comment