Maandalizi ya timu ya taifa ya England kwa ajili mashindano ya Mataifa ya Ulaya yamepata pigo kubwa kutokana ukweli kwamba watalazimika kuingia kibaruani dhidi ya Jamhuri ya Ireland, Finland na Ugiriki bila nyota wake Phil Foden, Cole Palmer, na Ollie Watkins.
Wachezaji hao muhimu katika kikosi cha England walikuwa wamejumuishwa awali katika kikosi cha kwanza kocha wa muda wa timu hiyo, Lee Carsley, lakini wamelazimika kujiondoa kutokana na sababu mbalimbali. Foden hakuripoti kambini kutokana na ugonjwa, wakati Palmer na Watkins wamerudi kwenye vilabu vyao kuendelea na matibabu yao ya majeraha madogo madogo yanayowakabili.
Suala hili limekuwa pigo kwa Carsley, ambaye amepewa jukumu la kuongoza England katika michuano ya Ligi ya Mataifa Ulaya, michuano itakayokuwa ya kwanza kwa England tangu kufungwa 2-1 na Hispania katika fainali za Euro 2024.
Foden, mchezaji muhimu wa Manchester City, amekuwa akipambana na ugonjwa na alikosa mechi za hivi karibuni za klabu yake dhidi ya Ipswich Town na West Ham United. Kukosekana kwake ni pigo kubwa kwa England kutokana na ubora wake.
Palmer na Watkins, ambao wote walikuwa sehemu ya kikosi cha England kwenye Euro 2024, wamekuwa wakikabiliana na matatizo ya majeraha yanayowasumbua kwa siku za hivi karibuni. Kutokuwepo kwao katika kikosi ni pigo kwa timu, kwani wote ni wachezaji wazuri wenye vipaji vikubwa.
Carsley sasa atalazimika kutathmini namna ya kufanya marekebisho kwenye kikosi chake kutokana na kuwakosa wachezaji hao muhimu ili kuhakikisha kwamba licha ya changamoto hii anaiongoza England kushinda katika mechi zao zijazo.
Kikosi cha England
Makipa: Dean Henderson (Crystal Palace), Jordan Pickford (Everton), Nick Pope (Newcastle United).
Walinzi: Marc Guehi (Crystal Palace), Ezri Konsa (Aston Villa), John Stones (Manchester City), Trent Alexander-Arnold (Liverpool), Levi Colwill (Chelsea), Rico Lewis (Manchester City), Tino Livramento (Newcastle), Harry Maguire (Manchester United).
Viungo: Conor Gallagher (Atletico Madrid), Kobbie Mainoo (Manchester United), Declan Rice (Arsenal), Morgan Gibbs-White (Nottingham Forest), Angel Gomes (Lille).
Washambuliaji: Jarrod Bowen (West Ham), Eberechi Eze (Crystal Palace), Jack Grealish (Manchester City), Anthony Gordon (Newcastle United), Harry Kane (Bayern Munich), Noni Madueke (Chelsea), Bukayo Saka (Arsenal).
Post a Comment